MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumanne, 31 Machi 2015

Filamu inayoangazia masaibu ya albino

                                  fuata hii filamu ujifunze kutokomeza mauaji ya albino

Familia ya Watoto 9 na ulemavu wa macho


Aliye waua Waingereza wawili kunyongwa

                                                   Kitanzi cha kunyongea watu

Wagombea urais Nigeria mchuano ni mkali

SKENDO WODINI: MAMA ADAI KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, APEWA WA KIKE TENA MAITI


MKUU WA WILAYA KINONDONI PAUL MAKONDA AMJULIA HALI ASKOFU GWAJIMA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akimjulia hali Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aliyelazwa Hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu baada ya kupata mshituko katika mahojiano na polisi akituhumiwa kutoa lugha isiyofaa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilibroad Silaa (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda walipokutana Hospitali ya TMJ walipofika kumjulia hali Askofu Gwajima.

KILICHOMPONZA ASKOFU GWAJIMA CHAJULIKANA

SOKO LA BUGURUNI: SHILINGI MIL.27 HUKUSANYWA KWA MWEZI, LAKINI HALI YA UCHAFU SOKONI HAPO NI HATAR

Jumatatu, 30 Machi 2015

MUSOMA VIJIJINI HUDUMA ZA AFYA, MAJI SAFI, ELIMU NI TATIZO KUBWA


Musoma Vijijini ni moja kati ya wilaya sita zinazounda Mkoa wa Mara. Upande wa Kaskazini, inapakana na Tarime na Musoma Mjini, Upande wa Mashariki, kuna Wilaya ya Sengerema, Kusini kuna Wilaya ya Bunda na Magharibi inapakana na Ziwa Victoria.
Mheshimiwa Nimrod Mkono.
Pia Musoma Vijijini ni jimbo la uchaguzi linaloongozwa na Mheshimiwa Nimrod Mkono kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Wiki iliyopita, Uwazi lilifunga safari hadi kwenye jimbo hilo ambalo kwa sasa makao makuu yake yapo Butiama na kuzungumza na wananchi mbalimbali walioeleza matatizo yanayowakabili.

MATATIZO YA WANANCHI
Matatizo yaliyoelezwa na wananchi kadhaa waliozungumza na gazeti hili, ni uduni wa elimu, ukosefu wa huduma bora za afya, kukosekana kwa maji safi na salama na ukosefu wa umeme jimboni humo kwa muda mrefu.


“Angalau Profesa Muhongo alipokuwa Wizara ya Nishati na Madini alikumbuka kwao kwa kutandaza nguzo za umeme sehemu mbalimbali, hata hivyo bado umeme haujawaka kwani kabla hajakamilisha kazi yake ndiyo sakata la Escrow likamuondoa madarakani, tunamuomba mbunge wetu atusaidie,” alisema Mwita Magafu, mkazi wa jimbo hilo.
Tatizo lingine kubwa linalowasumbua wananchi wa jimbo hilo, ni uduni wa elimu unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa vyumba vya madarasa, uhaba wa walimu, madawati na vifaa vya kujifunzia.  

Elias Kajana Majinge ni Chifu wa Kabila la Wajita ambapo katika mahojiano na gazeti hili, alisema maendeleo ya elimu katika jimbo hilo yapo chini sana na yanazidi kuzorota kila kukicha huku kukiwa hakuna jitihada zozote za kuinua kiwango cha elimu jimboni humo.


“Zaidi ya wanafunzi 80 husoma katika darasa moja katika shule za msingi. Matokeo ya shule za sekondari ni mabaya mno, kwa mfano mwaka 2013, kati ya wanafunzi 1587 waliofanya mtihani wa taifa wa kuhitimu kidato cha nne kutoka shule 17 za sekondari za kata, waliopata daraja la kwanza walikuwa saba tu,” alisema Majinge na kuongeza kuwa waliopata daraja la pili walikuwa 55, wakati daraja la tatu walikuwa 195, daraja la nne walikuwa 497, daraja sifuri walikuwa 628, hali inayotoa tafsiri halisi ya jinsi elimu ilivyo duni jimboni humo.

Majinge aliongeza kueleza kwamba wanafunzi wengi wa shule za msingi, huhitimu darasa la saba wakiwa hawajui kusoma wala kuandika.


“Shule nyingi hazina madawati, hakuna madarasa hakuna walimu, hata kama wapo hawaingii madarasani,” alisema  Majinge.Wananchi wa Musoma Vijijini walieleza pia kuwa kero nyingine inayowasumbua ni ukosefu wa huduma za afya, ambapo kuna kituo kimoja tu cha afya jimbo zima kiitwacho Murangi pamoja na zahanati kadhaa ambazo hata hivyo hazikidhi mahitaji ya wananchi wote wa jimbo hilo, huku kukiwa hakuna hospitali kubwa hata moja.

“Kama una mgonjwa wako amezidiwa, inabidi mumbebe kwenye machela kwenda Musoma Mjini au Bunda, huko ndiyo kuna hospitali, vinginevyo atakufa huku mkishuhudia, Kituo cha Afya cha Murangi hakina dawa wala wauguzi wa kutosha, hizo zahanati ndiyo usiseme. Tunaomba serikali itusaidie jamani,” alisema Marwa Mturo mkazi wa jimbo hilo.

“Pia hili jimbo lina migogoro mingi ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima na kuna wakati kuliwahi kutokea mapigano yaliyosababisha vifo. Tunamuomba Mkono atimize ahadi zake alizotuahidi wakati akiomba kura,” alisema Issa Rajab, mkazi wa Saragana.

Kero nyingine ambayo Uwazi iliibaini, ni ukosefu wa maji safi na salama licha ya kwamba jimbo hilo linapakana na Ziwa Victoria pamoja na Mto Mara. Wananchi wengi hunywa maji ya ziwani pamoja na ya kwenye mito, ambayo pia hutumika kunyweshea mifugo na kilimo jambo ambalo linaweza kuhatarisha afya zao.

Baada ya kusikiliza kero za wananchi, Uwazi lilimtafuta Mheshimiwa Mkono ambaye mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni, namba yake ya simu haikuwa ikipatikana hewani. Hata hivyo, jitihada za kumtafuta bado zinaendelea ili atoe ufafanuzi wa kero zilizoainishwa na wananchi wa jimbo lake.

MAMA AWAFUNGIA NDANI WANAYE 3 KWA MIAKA 10

IJUE THAMANI YA ASALI, NI CHAKULA,UREMBO NA NI DAWA

                                                 ASALI IKITUMIKA KWENYE MKATE

USINZIBE MDOMO: WANATAKA KUTUFUNGA, WENYEWE WANAJILINDA!

                                     Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Bunge lilipitisha sheria ya takwimu ya mwaka 2013, inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni 10 au vyote kwa pamoja kwa mwandishi au chombo cha habari kitakachotoa kimakosa takwimu za serikali wakati wakitekeleza wajibu wao.
                        Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju.
Sheria hiyo ya takwimu pia inazuia taasisi binafsi zilizokuwa zikikusanya na kutangaza takwimu za tafiti mbalimbali nchini kutofanya hivyo bila ya idhini ya mtakwimu mkuu wa serikali.

Sheria hizi zimetengenezwa ili kuwaziba midomo waandishi na watafiti binafsi wanaofanya kazi kwa masilahi ya nchi, ambao hukosoa taarifa potovu zinazotolewa na maofisa wa serikali katika idara mbalimbali.


Wakati serikali ikiwasilisha muswada huo ambao una ukakasi, sheria hiyo haisemi lolote juu ya ofisa wa serikali atakayetoa taarifa hizo potofu kwa mwandishi au chombo cha habari na hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju (pichani) alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alijibu kirahisi kuwa mwandishi au chombo cha habari vitalazimika kwenda kujieleza polisi au mahakamani.

Kwa maana nyepesi ni kuwa ofisa wa serikali, anaruhusiwa kudanganya, lakini uongo huo ukichukuliwa na mwandishi na kuandikwa, imekula kwake!

Huu ni uonevu tunaofanyiwa waandishi kwa lengo la kutuziba midomo, serikali haitaki takwimu sahihi zifahamike kwa umma, kwa sababu kama wao serikali basi hawataki kutoa takwimu, kwa nini wasiziachie taasisi binafsi zenye uelewa wa kufanya tafiti?


Wanaogopa tafiti pinzani kwa sababu zitawaumbua uongo wao, ndiyo maana wanataka wafanya tafiti wote lazima kwanza wapate kibali cha mtakwimu mkuu, ambaye kabla ya kutoa kibali, bila shaka ataweka mbele masilahi ya serikali na kutoa maelekezo.

Hivi ni vitisho ambavyo ni aibu kwa taifa linalojiita la kidemokrasia kama letu. Afadhali basi vikwazo kama hivi vinavyowekwa kwa wanahabari, vingewekwa pia kwa wezi wengi walio serikalini ambao kila siku wanafanya usanii na kuiba mabilioni, lakini hatuoni wakipeleka sheria bungeni za kuwabana.

Ninachotaka kuwakumbusha watawala ni kwamba siku zote hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho, watatufunga leo, lakini kesho na keshokutwa vizazi vyao vitalipia dhambi hii na sisi hatutaogopa kusema ukweli kwa sababu tunaitetea nchi ambayo wote tumeikuta!

MKUU WA WILAYA KINONDONI PAUL MAKONDA AKUTANA NA WANA UMOJA WA MAFUNDI MAGARI TEGETA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI DHIDI YA MWEKEZAJI‏

 DC Paul Makonda akiwahutubia wana umoja huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda…
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa na Viongozi wa Umoja wa Mafundi Magari Tegeta wakati akikagua eneo lenye mgogoro wa ardhi kati ya wanaumoja huo pamoja na mwekezaji alipokwenda kuwasikiliza kuhusu mgogoro huo Dar es Salaam jana.
 DC Paul Makonda akiwahutubia wana umoja huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa na viongozi wa umoja huo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Nationi Ndela akitoa historia ya mgogoro huo mbele ya DC Makonda.
 Baadhi ya mafundi magari katika gereji za Tegeta wakimsikiliza DC Makonda wakati akiwahutubia ili kupata muafaka wa mgogoro huo.
 Baadhi ya gereji zilizopo katika eneo hilo la mgogoro.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (katikati), akijaribu moja ya mashine ya kuchonga vyuma iliyopo katika eneo hilo.
 Baadhi ya mafundi na wamiliki wa gereji mbalimbali katika eneo hilo la mgogoro wakimsikiliza DC Makonda.
 Wanaumoja hao wakiwa kwenye mkutano huo.
Hapa DC Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Bunju B Kitunda ambao nao wanamgogoro na mwekezaji katika eneo hilo.
Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ameanza kufanya juhudu za makusudi za kujaribu kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya Umoja wa Mafundi Magari Tegeta dhidi ya mmoja wa wawekezaji wilayani humo.
Jitihada hizo ameanza kuzichukua ili kujaribu kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu na kudumaza shughuli za maendeleo katika eneo hilo la mgogoro lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana na mafundi eneo la  Tegeta zilipo gereji mbalimbali zinazo milikiwa na wanaumoja hao alitoa mapendekezo ya kukutana na viongozi wa umoja na mwekezaji ili kufanya mazungumzo ya pamoja kwa ajili ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo.

"Eneo hili tayari mahakama imemtambuwa mmiliki wake ambaye ndio mlalamikaji lakini hata hivyo kuna kila sababu ya kukutana na pande zote pamoja na mwekezaji huyo ili tupate ufumbuzi wa mgogoro huu ili uishe ili shughuli za maendeleo ziweze kuendelea" alisema Makonda.

Akizungumzia mgogo huo Naibu Katibu mku wa umoja huo Nationi Ndela alisema ni wa siku nyingi na kuwa kila wanapokwenda wamekuwa hawafanikiwi ambapo walimuomba mkuu huyo wa wilaya kuwasaidia.

Ndela alisema uwekezaji waliouweka katika eneo hilo unafikia zaidi ya sh.bilioni 35 hivyo ni vizuri serikali ikaliangalia jambo hilo kwa ajili ya kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa ndani.

Alisema kwamba mwekezaji anayedaiwa kumiliki eneo hilo alikuwa na kiwanda cha kutengeneza mabati aina ya asbesto na mara ya mwisho kufanya uzarishaji wa bati hizo ilikuwa kwenye miaka ya 70 tangu wakati huo eneo hilo lilikuwa wazi.

DC Makonda mbali ya kukutana na wamiliki wa gereji hizo pia alikutana na wananchi wa Bunju B Kitunda ambao nao wanamgogoro wa ardhi na mwekezaji ambapo aliwataka viongozi wa eneo hilo kufika ofisini kwake baada ya sikukuu ya pasaka ili kujua chanzo cha mgogoro huo.

Makonda ilikukabiliana na migogoro ya ardhi katika wilaya yake ameanzisha utaratibu wa kukutana na pande zinazovutana kila Ijumaa ili kuitafutia muafaka.
NA MTANDAO WA WWW.HABARI ZA JAMII.COM AMII

11 wauawa Brazil katika uporaji

Idara ya usalama nchini Brazil imesema kuwa imewaua watu saba waliokuwa wakifanya jaribio la kupora katika benk moja na ambao pia wanadaiwa kujiusisha na dawa za kulevya.

Taarifa hizo zinasema kuwa majambazi hao walianza kurushiana risasi na Polisi katika mji wa Novos Kaskazin Mashariki mwa Brazil.\

 Mtu mmoja anashikiliwa na Polisi,ambapo pia bunduki na vifaa vya milipuko vilivyokuwa vinamilikiwa na watu hao vinashikiliwa. Katika tukio jingine pia Polisi wamewaua watu wengine wanne wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya katika mji wa Rio de Janeiro.

 Kuuawa kwa majambazi hao kunafuatia mapambano ya polisi na kundi hilo,ambapo mabomu na Bunduki vilikamatwa pia

Hatima ya mpango wa nyuklia wa Iran leo


Matokeo ya uchaguzi Nigeria leo jioni

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.


Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura auli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011
.
 Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi."

Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. 

Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega.

Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo.

Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.

Jumapili, 29 Machi 2015

Alhamisi, 26 Machi 2015


Mauaji ya Albino ni aibu kwa Tanzania




ASKARI WAWILI MBARONI KWA FEDHA BANDIA

> Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo akionyesha sare za jeshi la wananchi zilizokamatwa kutoka kwa askari polisi baada ya kupekuliwa nyumbani kwake. Picha na Faustine Fabian 
Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo alisema askari hao walikamatwa juzi saa tisa mchana katika Mtaa wa Old Maswa, Kata ya Nyakabindi, wilayani Bariadi.
Alisema askari hao walifika kwenye kibanda cha Mpesa kinachomilikiwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old Maswa, Kassian Luhende (29) wakiwa na pikipiki aina ya Sunlg kwa lengo la kuweka fedha hizo katika simu.
Alisema baada ya mwalimu huyo kupokea noti 10 zenye thamani ya Sh100,000 alizitilia shaka na kuamua kuzikagua zaidi ndipo alipogundua kuwa siyo fedha halali.
Mkumbo alisema mwalimu huyo baada ya kugundua hilo aliomba msaada wa kukamatwa kwa askari hao. Alisema majirani walipofika walihoji, ndipo mmoja wao alipotoa kitambulisho kuwa yeye ni askari na mwingine kujitambulisha kuwa ni dereva bodaboda.
Alibainisha kuwa baada ya wananchi kuambiwa hivyo waliwatilia shaka zaidi na kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Bariadi na kisha kukamatwa.
Mkumbo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari mwenye namba H 2420 PC Seleman Juma (25) ambaye ni wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Simiyu, na mwenye namba B.6499 WDR Edmund Masaga (28) wa Magereza wilayani Bariadi.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa, baada ya askari hao kukamatwa mmoja wao PC Selemani alipopekuliwa katika mfuko wa suruali yake, alikutwa na noti nyingine za bandia za Sh100,000.
Mbali na hilo Mkumbo alisema askari huyo alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na sare za JWTZ ambazo ni kaptula nne, fulana mbili, kombati moja pamoja na kitambaa.
Alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa usambazaji wa noti bandia ndani ya mkoa na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika askari hao watachuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kisheria.
                Na Faustine Fabian

Kwa nini rais ajaye awe mwanamke

> Mkurugenzi wa kituo cha Haki za Binadamu (LHRC),Dk Hellen Bisimba.
Wanaharakati nchini wamesema rais ajaye anaweza kuwa mwanamke kutokana na sababu kadhaa, ikiwamo wingi na hamasa waliyonayo wanawake katika upigaji kura.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema ingawa wanatambua uchaguzi ni mapambano, wanaamini kama wanawake na jamii itakubali mabadiliko, nchi itaongozwa na rais mwanamke.
Wanaharakati hao kutoka vyama vya Umoja wa Wanawake Wanasiasa (Ulingo), Mtandao wa Jinsia Tanzania, (TGNP), Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) walisema hakuna kinachoshindikana kama wanawake wataamua.
Ulingo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wanasiasa Tanzania (Ulingo), Anna Abdallah alisema, baada ya wanawake kuangaliwa kama kundi duni katika nyanja za siasa kwa muda mrefu, sasa ni zamu yao kujitokeza wagombee nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwamo ya urais.
“Lengo letu sisi ni mwanamke kujitokeza, akijitokeza tutamuunga mkono kwa umoja wetu bila kujali anatoka chama gani cha siasa,” alisema mwenyekiti huyo aliyeeleza kuwa jamii ya sasa ina imani kubwa na mwanamke.
Aliongoza “Iwapo wanawake watafanya kile tunachotaka , kwa maana ya kuwaunga mkono wagombea, kupiga kura, wakati wa kupata rais mwanamke umefika. Hilo halina ubishi na linawezekana.” Anna alitaja sababu nyingine za kuwashawishi wanawake wajitokeze kugombea urais kuwa ni kuongezeka kwa uelewa wa wanawake katika masuala ya siasa.
TGNP
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, (TGNP), Lilian Liundi alisema wanawake kuwa viongozi siyo ajabu kwani tayari wameshafanya hivyo katika nafasi mbalimbali. Isipokuwa wanahitaji kuungwa mkono katika nafasi za kisiasa.
Alisema mtandao huo utamuunga mkono mwanamke yeyote atakayeonyesha nia ya kugombea bila kuangalia itikadi ya chama anachotoka, huku ukiamini kuwa wanawake wanaweza kufanya vizuri zaidi wanapopata nafasi.
“Japokuwa historia inaonyesha wanafanya vizuri, tunahitaji kuwaunga mkono kwa nia thabiti ili wakalete mabadiliko ya kweli, ” alisema Liundi.

Baba mbaroni kwa kuwabaka watoto wake


UN YAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA WAATHIRIKA WA BIASHARA YA UTUMWA

TAHARIRI: TABIA HII YA WAUZA MITUMBA SOKO LA MCHIKICHINI NI UDHALILISHAJI WA KIJINSIA‏

MTOTO WA AJABU AZALIWA SHINYANGA