MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumamosi, 2 Aprili 2016

DIWANI VITI MAALUMU AANDAA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA CHUMBA CHA UPASUAJI.

Diwani wa viti Maalum kata ya Malampaka Pili Ndimila (mwenye gauni la mabaka ya njano na mke wa Mbunge mwenye koti jekundu Mama Mashimba) wakiungana na wanawake wenzao kubeba mawe kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa chumba cha upasuaji kituo cha afya Malampaka


Gari likishusha mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji kituo cha afya Malampaka iliyotolewa na Mashimba Ndaki Mbunge Jimbo la Maswa Magharibi.


KUFUATIA kukosekana kwa jengo la upasuaji katika kituo cha afya cha Malampaka hali iliyokuwa ikigharimu maisha ya akina mama wajawazito wilayani Maswa mkoani Simiyu,diwani wa viti maalumu wilayani hapo,Pilli Ndimila amefanya harambee kuchangia ujenzi huo.

Katika harambee hiyo iliyoambatana na maandamo ya wakinamama waliokuwa wamebeba mawe kuunga mkono juhudi za kiongozi wao,kukamilisha ujenzi huo ili  kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kupata huduma hiyo.

Akizungumza alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakifia njiani wakati wakisafirishwa kwenda maswa kwa ajili ya upasuaji wakati wa kujifungua kwa umbali wa kilomita 30 kutoka malampaka huku yeye kama mwanamke na akiwa kama mzazi anaguswa na tatizo hilo na kuamua kuitisha changizo.

‘’akina mama tunateseka kwa kufia njiani wakati tukienda hospitali kujifungua…mimi kama mwanamke na diwani, niliwiwa kuona wanawake wanakufa njiani nikaona ni vyema kuanzisha changizo kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji ili huduma hii ipatikane kwa ukaribu’’ alisema Ndimila.

Aliongeza kuwa wakinamama wengi wamekuwa wakifia njiani kutokana na ukosefu wa gari la wagonjwa na kumwomba makamu wa Rais mama Samia Suluhu kuunga mkono juhudi za wakinamama hao ili kuokoa maisha ya wanawake wa malampaka.


Mbunge wa maswa magharibi,Mashimba ndaki alisema vifaa vya upasuaji tayari vimeshaletwa na kufungiwa katika chumba maalumu na haviwasaidii wakazi wa malampaka.

Alisema kuwa kituo hicho kinahudumia wananchi wa kata hiyo na kata zingine tano zinazoizunguka malampaka huku wananchi wengi wakikosa huduma ya upasuaji na kulazimika kuifuata katika Hospitali ya Maswa.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Maswa Jonathani Budenu alisema kuwa wananchi wamekuwa wakisafirishwa umbali wa kilomita 30 kwa ajili ya kupata huduma ya upasuaji na kuwataka wananchi wasiishie hapo katika kuchangia pia watakapohitajika tena wajitokeze.


Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria katika changizo hilo wamesema kuwa wanafurahi kuona kiongozi mwanamke akitambua changamoto yao na kujua namna ya kuitatua ili kuondoa vifo visivyo vya lazima huku baadhi yao walikuwa wakifia njiani kabla ya kufika maswa hospitalini.

“wanawake tumekuwa tukihangaika wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma ya upasuaji na wengine kufia njiani wakati wakienda kupata huduma katika hospitali ya wilaya ya maswa…na sisi wanawake leo tumejitokeza tumebeba mawe kuunga mkono juhudi za diwani wetu Pili Ndimila” alisema Pendo Joseph mkazi wa Malampaka.


Wananchi wa malampaka walikuwa wanasafiri umbali wa kilometa 30 ili kupata huduma ya upasuaji katika hospitali ya wilaya ya maswa, kufuatia changizo hilo la ujenzi wa chumba cha upasuaji mbunge wa jimbo la maswa magharibi alitoa mifuko I00 ya sariju na kufanya  jumla ya mifuko 280 ya saruji iliyochangwa, huku ahadi ikiwa ni mifuko 64 na fedha shilingi 445,500 huku ahadi ikiwa ni 560,000.
NA HARUA UJUKU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni