MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Alhamisi, 26 Machi 2015


Imeelezwa kuwa kitendo cha wananchi wengi kukosa elimu ya kiroho inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe katika mkoa wa Shinyanga.

 Hayo yamesemwa  na katibu wa Chama Cha Watu wenye Ulemavu wa ngozi katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Seif Rashid wakati wa majadiliano maalum na waandishi wa habari yaliyoandaliwa na TGNP Mtandao yaliyofanyika mjini Shinyanga.



Rashid amesema vitendo vya mauaji vinafanywa na watu wasiokuwa na hofu ya mungu hivyo kuzitaka taasisi za kidini kuwapa elimu ya kiroho ili kutokomeza mauaji katika jamii.
Amesema kitendo cha wananchi kukosa hofu ya mungu ndicho kinawafanya wakimbilie kwa waganga wa kienyeji wakiamini kuwa watatatuliwa matatizo yao.
 
 Amesema mbali na kukosa elimu ya kiroho,wananchi wengi hawana elimu dunia,matokeo yake wanawaamini waganga wa jadi kupitia ramli zao,vitendo ambavyo vinachangia mauaji ya watu wasio na hatia kwani waganga  wengi wa jadi wanafanya ramli chonganishi.
 
 Nao baadhi ya wananchi wa  wilaya ya Kishapu waliohudhuria majadiliano hayo wamesema changamoto iliyopo wilayani Kishapu ni ubaguzi wa rangi katika jamiii ambapo watoto wenye rangi nyeupe wanaonekana kuwa na thamani zaidi ya watoto wenye rangi nyeusi.
 
 Wamesema hivi sasa watoto wenye rangi nyeupe wanalazimishwa kuolewa ili wazazi wapate ng’ombe kuanzia 25-35 na wenye rangi nyeusi wakiolewa kwa ng’ombe 4 hadi 10 huku wengine wakikatishwa masomo yao.
 
 
Naye afisa program,utafiti na uchambuzi kutoka TGNP Mtandao Deogratius Temba amekemea kitendo cha watoto kuachishwa masomo ili waolewe na ameitaka jamii kubadilika na kuacha kubagua watoto kwani kufanya hivyo ni kuendeleza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
             
   Na NEEMA RUBEN
                        ----mwisho--

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni