Gari
likishusha mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji
kituo cha afya Malampaka iliyotolewa na Mashimba Ndaki Mbunge Jimbo la Maswa
Magharibi.
KUFUATIA kukosekana kwa jengo la
upasuaji katika kituo cha afya cha Malampaka hali iliyokuwa ikigharimu maisha
ya akina mama wajawazito wilayani Maswa mkoani Simiyu,diwani wa viti maalumu wilayani
hapo,Pilli Ndimila amefanya harambee kuchangia ujenzi huo.
Katika harambee hiyo iliyoambatana
na maandamo ya wakinamama waliokuwa wamebeba mawe kuunga mkono juhudi za
kiongozi wao,kukamilisha ujenzi huo ili
kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kupata huduma hiyo.
Akizungumza alisema kuwa wanawake
wengi wamekuwa wakifia njiani wakati wakisafirishwa kwenda maswa kwa ajili ya
upasuaji wakati wa kujifungua kwa umbali wa kilomita 30 kutoka malampaka huku
yeye kama mwanamke na akiwa kama mzazi anaguswa na tatizo hilo na kuamua
kuitisha changizo.
‘’akina mama tunateseka kwa kufia
njiani wakati tukienda hospitali kujifungua…mimi kama mwanamke na diwani,
niliwiwa kuona wanawake wanakufa njiani nikaona ni vyema kuanzisha changizo kwa
ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji ili huduma hii ipatikane kwa ukaribu’’
alisema Ndimila.
Aliongeza kuwa wakinamama wengi wamekuwa
wakifia njiani kutokana na ukosefu wa gari la wagonjwa na kumwomba makamu wa
Rais mama Samia Suluhu kuunga mkono juhudi za wakinamama hao ili kuokoa maisha
ya wanawake wa malampaka.
Mbunge wa maswa magharibi,Mashimba
ndaki alisema vifaa vya upasuaji tayari vimeshaletwa na kufungiwa katika chumba
maalumu na haviwasaidii wakazi wa malampaka.
Alisema kuwa kituo hicho kinahudumia
wananchi wa kata hiyo na kata zingine tano zinazoizunguka malampaka huku
wananchi wengi wakikosa huduma ya upasuaji na kulazimika kuifuata katika
Hospitali ya Maswa.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa
wilaya ya Maswa Jonathani Budenu alisema kuwa wananchi wamekuwa wakisafirishwa
umbali wa kilomita 30 kwa ajili ya kupata huduma ya upasuaji na kuwataka
wananchi wasiishie hapo katika kuchangia pia watakapohitajika tena wajitokeze.
Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria
katika changizo hilo wamesema kuwa wanafurahi kuona kiongozi mwanamke akitambua
changamoto yao na kujua namna ya kuitatua ili kuondoa vifo visivyo vya lazima
huku baadhi yao walikuwa wakifia njiani kabla ya kufika maswa hospitalini.
“wanawake tumekuwa tukihangaika
wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma ya upasuaji na wengine kufia njiani
wakati wakienda kupata huduma katika hospitali ya wilaya ya maswa…na sisi
wanawake leo tumejitokeza tumebeba mawe kuunga mkono juhudi za diwani wetu Pili
Ndimila” alisema Pendo Joseph mkazi wa Malampaka.
Wananchi wa malampaka walikuwa
wanasafiri umbali wa kilometa 30 ili kupata huduma ya upasuaji katika hospitali
ya wilaya ya maswa, kufuatia changizo hilo la ujenzi wa chumba cha upasuaji
mbunge wa jimbo la maswa magharibi alitoa mifuko I00 ya sariju na kufanya
jumla ya mifuko 280 ya saruji iliyochangwa, huku ahadi ikiwa ni mifuko 64 na
fedha shilingi 445,500 huku ahadi ikiwa ni 560,000.
NA HARUA UJUKU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni