CHAKULA CHA MSAADA KINAVYOWANUFAISHA VIONGOZI
MKUU wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu,Paunsiano Nyami
amemsimamisha kazi Mtendaji wa kata ya Somanda wilayani hapo,Joseph Shabalanga
kwa kosa la kutorosha gunia 6 za mahindi ya msaada katika ngala la chakula
hicho.
Alieleza kuwa Mtendaji huyo,alitokomea kusiko julikana baada
ya chakula hicho kukamatwa mpaka Mkuu huyo wa wilaya alipoamua kutumia lugha za
kumshawishi kuwa hawezi kuwa na hatia kwa njia ya simu hali ailiomsababisha mtendaji
huyo ajisalimishe kwa jeshi la polisi.
Akizungumza Nyami alisema mnamo tarehe 11 february magunia 6
ya mahindi yalitorosha na watu wasiojulikana pasipo kujua ni njia gani
zilitumika kutorosha chakula hicho kIsha February 12 majira ya saa 6 usiku
baadhi ya magunia 6 ya chakula hicho yalishikwa maeneo ya Somanda Mkoani hapo.
Nyami akiyabainisha yaho juzi ofisini kwake alisema kuwa
jeshi la polisi wilayani hapo
liliwakamata wenyeviti wa mitaa kata ya somanda
kwajili ya upelelezi huku wakiwawameweka ndani mlinzi wa mahakama ya
somanda,Sitta Burugu,Anna Shushi mtendaji wa kata ya Nyaumata na Salome
Masalila mtendaji wa mtaa Somanda.
NA MWANDISHI WETU
“Mh waziri jenista alifofika kuangalia hali ya njaa katika
Mkoa wetu aliahidi kuleta chakula mapema na baada ya muda kweli
kilifika.chakula hiki kilikuwa ni kwajili ya watu ambao hawajiwezi kabisa..wale
maskini ambao hawajiwezi kwa kila kitu ndio ambao tunawapatia chakula
hiki”Alisema.
“Mtazamo wa suala hili ni wizi tumejaribu kumtafuta
aliyeuziwa magunia hayo 6,mpaka sasa bado hajaoneka ila tumemtambua ni
mfanyabiashara wa duka maeneo ya somanda anaitwa,Shulinde”Aliongeza.
Aidha alisema kuwa katika halmashauri ya wilaya Bariadi
walipokea tani 70 nahalmashauri ya Mji ikipokea tani 51.01 kwajiri ya chakula
hicho cha msaada.
Sambamba na hayo Nyami ametoa wito kwa viongozi
waliochaguliwa na wanachi kuwa waadilifu katika kazi kwa kuzingatia sheria na
kwa watakao kiuka taratibu hatasita kuwachukulia hatua za kisheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni